Mhe. Balozi Fredrick I Kibuta, Balozi wa Tanzania nchini Russia amekutana na Wanachama wa Jumuiya ya Diaspora raia wa Tanzania nchini Russia mnamo tarehe 26 Machi 2022 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo jijini Moscow, Russia kwa njia ya mtandao.
Mhe. Balozi alitumia fursa ya kikao, pamoja na mambo mengine kujitambulisha rasmi kwa wanachama wa Jumuiya ya Diaspora waliopo nchini Russia na nchi huru za Jumuiya ya Madola ( Common Wealth of Independent States- CIS) .
Kupitia ratiba ya kikao hicho, Mhe. Balozi alipata fursa ya kumuapisha Katibu Mpya wa Jumuiya, aidha, kulingana na Katiba ya umoja huo ambayo inaelekeza kufanyika uchaguzi wa viongozi kwa mwaka unaofuata, Mhe. Balozi alisimamia mchakato wa kupendekeza majina matano ya wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi. Kamati hii itasimamia mchakato wa kupatikana kwa viongozi wapya wa Jumuiya ya Diaspora
Wakati wa majadiliano masuala mbalimbali yaliibuliwa na majibu ya hoja mbalimbali yalitolewa na maafisa wa ubalozi kwa kushirikiana na uongozi wa Diaspora.
Mkutano huu ulitumika kuhamasisha Jumuiya ya Diaspora kuzichangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana nchini Tanzania
Ubalozi wa Tanzania Moscow
Tarehe 26 Machi 2022
#kaziiendeleee