Ubalozi wa Tanzania Moscow uliadhimisha siku ya lugha ya kiswahili duniani tarehe 7 Julai 2022. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Waheshimiwa Mabalozi wa EAC, Chama cha Kiswahili Moscow (CHAKIMO), Diaspora na Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Itakumbukwa kuwa UNESCO ilitangaza siku ya Julai 7 kila mwaka kuwa siku rasmi ya kuadhimisha Lugha ya Kiswahili ulimwenguni.


Ubalozi wa Tanzania
Moscow