Balozi wa Russia nchini Tanzania Mhe. Andrey Avetsyan, amekutana kwa mazungumzo na Mhe. Fredrick I Kibuta, Balozi wa Tanzania nchini Russia. Mazumgumzo hayo yamefanyika leo tarehe 12 Aprili 2022 katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo jijini Moscow ambapo pamoja na mambo mengine, Urusi imeahidi kuongeza fursa zaidi za masomo ya Elimu ya Juu kila mwaka kwa wanafunzi wa Tanzania, sambamba na hilo , Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kupitia biashara, kuvutia wawekezaji na kuongeza idadi ya watalii. halikadhalika, kueneza lugha ya kiswahili pamoja na kutangaza utamaduni kwa maslahi mapana ya nchi hizi mbili.