Balozi Kibuta amekutana na viongozi wa Chama cha Kiswahili Moscow ambao pia ni waalimu wa Lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Serikali cha Moscow ( Moscow State University) na Chuo Kikuu cha Mahusiano ya Kimataifa( Moscow State University of International Relations). Mazungumzo haya yamefanyika ikiwa ni utekelezaji wa Mpango kazi wa kukuza na kueneza Lugha ya kiswahili kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kiswahili ifikapo tarehe 7 Julai 2022. Lengo ni kujadili mwenendo wa ufundishaji wa Kiswahili kwenye vyuo hivi viwili pamoja na kupanga mikakati wa kufundisha kiswahili katika vyuo vingine ambavyo ni Chuo Kikuu cha St’ Petersburg na Chuo Kikuu cha Serikali cha Kazan( Kazan State University. Katika kikao hicho zilijadiliwa changamoto na mafanikio na namna bora ya kuboresha zaidi masuala mbalimbali yanayohusu kueneza Lugha ya Kiswahili nchini Russia