Tarehe 12 -13 Mei, 2025 Wizara kupitia Ubalozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji ilishiriki katika Mkutano wa Pili wa  Tume ya pamoja ya ushirikiano wa Biashara na Uchumi kati ya Tanzania na Urusi Mjini St. Petersburg Urusi. Lengo la Mkutano huo pamoja na mambo mengine ni kujadili kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa kwanza uliofanyika Mwezi Oktoba, 2024 Dar es Salaam, Tanzania.  Aidha, Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji ambapo ujumbe wa Shirikisho la Urusi uliongozwa na Mhe.Maxim Reshetnikov, Waziri wa Maendeleo ya Uchumi. Kupitia Mkutano huo, Viongozi hao wamesaini makubalino yaliyoainisha masuala muhimu ya utekelezaji baina ya pande hizo mbili ili kuweza kufikia malengo ya ya Mkataba wa Tume hiyo. Masuala hayo yamejumisha sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, Kilimo, Viwanda,Utalii, Madini, Nishati  na Biashara. Vilevile, Mkutano huo ulihusisha ushiriki wa Wafanyabashara wa Tanzania na Urusi ambao walipata nafasi ya kukutana na kujadiliana kuhusu namna bora ya kushirikiana katika masuala ya Uwekezaji na Biashara. Mkutano wa Tatu wa Tume hiyo umepangwa kufanyika Tanzania kwa tarehe zitakazopangwa hapo baadae.