Ubalozi kwa kushirikiana na Kampuni ya ndege ya Qatar ulifanya Semina ya Utalii  wa Tanzania tarehe 13 Novemba 2019 katika Ukumbi wa Mkutano wa Ubalozi. Kampuni ya ndege ya Qatar walitoa wasilisho kuhusu kuongeza safari zao Tanzania ambapo sasa wanatua Dar es Salaam, Zanzibar na Kilimanjaro, sehemu ambazo watalii wengi hupenda kutembelea. 

Mhe. Balozi Mej. Jen. (Mst.) Simon M. Mumwi alitoa hotuba ya ufunguzi ambapo katika hotuba yake alielezea aina mbali mbali za vivutio vilivyopo Tanzania.  Washiriki katika Semina hiyo walikuwa Wadau mbali mbali kutoka Kampuni za Urusi zinazojishughulisha na Biashara ya Utalii.

  • Washiriki wakimsikiliza Mhe. Balozi wakati akielezea vivutio vilivyopo Tanzania katika Hotuba yake