Tarehe 22 Mei 2019 kwa kushirikiana na Wanafunzi wanaosoma jijini Moscow,  Ubalozi ulishiriki kwenye siku ya Utamaduni iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Ufundi "Moscow Politech". Katika tafrija hiyo kulifanyika Maonesho ya Vyakula vya asili, Ngoma za asili pamoja na kuonesha mavazi ya asili ya Tanzania. 

Ubalozi uliweza kutumia fursa hiyo pia kutangaza Utalii wa Tanzania kwa kutoa majalada mbali mbali yanayoonesha vivutio vya Utalii vilivyopo Tanzania, kama vile Mbuga za wanyama na kisiwa cha Zanzibar. 

  • Mhe. Balozi Maj Gen (Mst.) Simon Mumwi akisoma hotuba katika tafrija hiyo.
  • Wanafunzi wa Kitanzania wakitoa Historia fupi ya Tanzania pamoja na kumzungumzia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
  • Wanafunzi wa Kitanzania wakicheza ngoma za utamaduni wa Kitanzania
  • Mhe. Balozi Mumwi pamoja na waalikwa wengine wakiangalia watumbuizaji katika hafla hiyo
  • Mhe. Balozi Maj. Gen (Mst) Simon Mumwi pamoja na Bi Asha Mkuja, Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wakiangalia vyakula vyenye asili ya kitanzania
  • Picha ya pamoja ya wanafunzi walioshiriki katika hafla hiyo.