Mhe Balozi Fredrick Ibrahim Kibuta, Balozi wa Tanzania katika Shirikisho la Urusi akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi 11 kutoka Chuo Kikuu Sumy Ukraine baada ya kuwapokea kutoka Ukraine. Takribani wanafunzi 83 wamekwama nchini Ukraine kutokana na mgogoro kati ya Shirikisho la Urusi na Jamhuri ya Ukraine, Jitihada zinaendelea ili kuwaokoa wanafunzi wengine waliobaki nchini Ukraine. Aidha, Taratibu za kuwarejesha Tanzania wanafunzi hawa 11 kwa kushirikiana na familia zao tayari zimeanza. Moscow 08 Machi 2022