Mhe. Balozi Fredrick I. Kibuta amekutana kwa mazungumzo na Mhe. Prof. Dkt. Jose’ M. Katupha, Balozi wa Jamhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa SADC nchini Russia.  Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 17 Machi 2022 katika Ubalozi wa Msumbiji uliopo jijini Moscow. Pamoja na mambo mengine, masuala mbalimbali ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Msumbiji yalijadiliwa. Mhe. Kibuta alitumia fursa ya mazungumzo kumpongeza balozi wa Msumbiji kwa uongozi wake mahiri katika kutekeleza masuala mbalimbali yanayohusu maslahi mapana ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC ikiwemo Tanzania. Vile vile alimshukuru kwa Ushirikiano aliompatia wakati wa zoezi la kuwanasua wanafunzi wa Tanzania waliokwama nchini Ukraine kufuati mzozo kati ya Shirikisho la Urusi na Jamhuri ya Ukraine. Katika mazungumzo yao  waligusia masuala kadhaa ikiwemo jitihada za ukanda wa SADC na Nchi hizi mbili za kukabiliana na matukio ya ugaidi nchini Msumbiji. Aidha, wameahidiana kushirikiana zaidi ili kufanikisha majukumu yao.