Mhe. Fredrick Ibrahim Kibuta, Balozi wa Tanzania nchini Russia ameungana na waombalezaji mbalimbali katika kusaini kitabu cha maombolezo cha aliyekuwa Raisi wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Raisi Rupiah Bwezani Banda. Tukio hilo limefanyika leo tarehe 17 Machi 2022 katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Zambia jijini Moscow. Mhe Balozi Aliwasilisha Salam za pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Zambia na kwa Wazambia wote kwa kufikwa na msiba huu mkubwa. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Hayati Rais Banda Mahala pema peponi Amini