Mhe. Balozi Fredrick I. Kibuta, Balozi wa Tanzania nchini Russia amekutana kwa mazungumzo na Mhe. Balozi Ben H.O Ogutu Balozi wa Jamhuri ya Kenya nchini Russia na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa EAC.
Masuala mbalimbali yanayohusu mahusiano na ushirikiano katika sekta za uchumi, biashara na diplomasia baina ya Tanzania na Kenya yamejadiliwa.
Sambamba na hayo, waliahidiana kushirikiana ili kutekeleza majukumu yao katika Shirikisho la Urusi.
#Kazi Iendelee
TArehe 21 Machi 2022
Russia