Mhe. Balozi Frederick Ibrahim Kibuta, Balozi wa Tanzania katika Shirikisho la Urusi amekutana kwa mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Kiswahili Moscow (CHAKIMO) leo tarehe 04 Machi 2022. katika Ofisi za Ubalozi zilizopo jijini Moscow.

Pamoja na mambo mengine, Mhe Balozi ameufahamisha ujumbe huo kuhusu azma ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kufungua matawi mengi zaidi ya kufundisha lugha ya Kiswahili nchini Urusi. Aidha, pamoja na kuwapongeza viongozi wa chama hicho kwa kazi kubwa inayoendelea ya kuitangaza kimataifa lugha ya kiswahili amewahakikishia kuwapa Ushirikiano wa hali na mali katika kuzitatua changamoto zote ili kuhakikisha Lugha hii nzuri na ya kihistoria inawafikia watu wengi zaidi katika maeneo yote ya uwakilishi.