Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Shirikisho la Urusi, Diaspora wamepata elimu ya uzalendo na namna ambavyo wanaweza kuchangia kuongeza fursa mbalimbali kutoka katika  Shirikisho la Urusi  ikiwemo utalii, masoko, uwekezaji, afya na elimu. Ubalozi wa Tanzania Moscow umeandaa semina hii ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara.