Ubalozi ukishirikiana na Balozi nyingine wanachama wa Umoja wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zilizopo jijini Moscow ulisherehekea miaka 27 ya kuanzishwa kwa Umoja huo. Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 19 Septemba 2019 hapa Moscow. Mhe. Balozi Mej Jen (Mst.) Simon M. Mumwi, Balozi wa Tanzania katika Shirikisho la Urusi na  Mwenyekiti wa Mabalozi wa nchi za SADC zilizopo Moscow alitoa Hotuba ya ufunguzi wa Sherehe hiyo. 

Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa Balozi Andrey Kemarsky, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Shirikisho la Urusi. Waalikwa katika Sherehe hiyo walikuwa Mabalozi wa nchi mbali mbali wanaowakilisha nchi zao katika Shirikisho la Urusi, Maofisa wa Serikali ya Urusi, Viongozi wa Vyuo na Taasisi za Elimu, Mashirika binafsi yakiwemo yanayojishughulisha na Utalii pamoja na wafanyabiashara.

  • Mhe. Balozi Mumwi akimpa zawadi ya Jarida la Maendeleo ya nchi za SADC Balozi Andrey Kemarsky lililotolewa katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC uliofanyika mwezi Agosti 2019 jijini Dar Es Salaam
  • Picha ya pamoja ya Mabalozi wa nchi za SADC
  • Wanafunzi wa Kitanzania wakitumbuiza kwa ngoma za Kitanzania katika Sherehe hiyo